WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamempa siku 15 Mweka Hazina wa Wilaya ya Sikonge, Bw. Evans Shemdoe ajieleze nikwa nini ameshindwa kufikisha asilimia 80 ya makusanyo ya ndani.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Alhamisi, Agosti 10, 2017 wakati akizungumza na watumishi nawatendaji wa wilaya hiyo, mjini Sikonge wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Tabora..
“Nataka maelezoyakayoniridhisha ni kwa nini hamkufikisha asilimia 80 ya makusanyo yahalmashauri ambacho ni kiwango cha chini. Nzega TC wamefikisha asilimia 112,Kaliua wana asilimia 91, Nzega DC wana asilimia 80, ni kwa nini wewe umeshindwakufikisha kiwango hicho?,” alihoji Waziri Mkuu.
“Ninataka nipate maelezo piani ipi mipango yenu ya kukusanya mapato kwa maeneo mliyoshindwa kufanya vizuri,na pia mmejipangaje kwa mwaka ujao wa fedha. Niyapate maelezo hayo ifikapotarehe 25 Agosti,” amesema.
Alipopewa nafasi yakujieleza, Bw. Shemdoe alisema wamefikisha asilimia 76.7 na wameshindwa kufikialengo kwa sababu ya upungufu wa mvua katika msimu uliopita, hali ambayoilichangia kushuka kwa mavuno ya zao la tumbaku miongoni mwa wakulima.
Hata hivyo, Waziri Mkuualiwataka watumishi wa wilaya hiyo, washirikiane na watendaji na madiwani ilikuongeza mapato ya wilaya hiyo badala ya kuwaachia watendaji wa kata peke yao.
Mara baada ya kupokea taarifaya mkoa wa Tabora, Waziri Mkuu alizitaka Halmashauri tano kati ya nane za mkoahuo zitoe maelezo ni kwa nini zimeshindwa kufikisha asilimia 80 ya makusanyokama ambavyo waliagizwa na Serikali.
“Halmashauri zilizovukamalengo ni tatu tu, Nzega TC, Kaliua na Nzega DC. Nataka taarifa za halmashaurizilizobakia ifikapo Agosti 25, wakijieleza ni kwa nini hawajafikia malengo yaukusanyaji mapato yaliyowekwa ambayo ni asilimia 80,” alisema.
Taarifa ya mkoa huoinaonyesha makusanyo kwa kila Halmashauri ni kama ifuatavyo:- Tabora Manispaaasilimia 64.1; Nzega Mji (asilimia 112); Nzega Wilaya (asilimia 80.8); Igunga(asilimia 64.6); Tabora (asilimia 77.3); Sikonge (asilimia 76.7); Urambo(asilimia 70.9) na Kaliua (asilimia 91.5).
Pia amezitaka Halmashaurizote zihakikishe zinafanyamakusanyo kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.“Ukusanyaji wote wa mapato ni lazima ufanyike kwa mfumo wa kielektroniki.Halmashauri ambazo hazijafanya hivyo, zitumie makusanyo ya mwaka jana kununuliamashine za EFD. Hatutaki kuona risiti za kuandika kwa mkono zinatumika,”alisisitiza.
Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa mkoa wa Tabora uhakikishe wanapatikanawatumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika wilaya hiyo ili wawezekusaidiana na watendaji wa halmashauri hiyo kukusanya mapato.
“Hapa Sikonge naambiwa hakunaofisi za TRA. Lazima tupate maafisa wa TRA katika kila Halmashauri ili watoeelimu na washirikiane na madiwani, watendaji wa vijiji na watumishi waHalmashauri juu ya ukusanyaji mapato,” alisema.
Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO